Ulinzi waongezwa Tamil Nadu, kiongozi wao afariki dunia

Jayalalitha Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jayalalitha

Polisi wa ziada wameongezwa katika jimbo la Tamil Nadu, kusini mwa India, kufuatia kifo cha mmoja ya wanasiasa maarufu nchini humo Jayalalitha.

Mamlaka nchini humo zinahofia kutokea vurugu miongoni mwa wafuasi wake ambao walikuwa wakimtii kwa kiasi kikubwa, kiasi cha kumpa heshima ya jina la Mama.

Kifo chake kilichotokana na Ugonjwa wa moyo katika hospitali iliyoko Chennai, kilitangazwa jana usiku.

Waziri mkuu wa India Narendra Modi, ametuma salamu za rambirambi akisema kwamba akisema kwamba kuguswa kwake na masuala ya wanawake, masikini na watu wengine wa pembezoni siku zote ni jambo litakalo kuwa mfano wa kuigwa.

Mwaka 2014 Jayalalitha alikutwa na hatia ya rushwa, lakini baadaye alirejea tena katika majukumu yake ya kazi kama mkuu wa jimbo la Tamil Nadu.