Maelfu waomboleza kifo cha 'Iron Lady' wa India Jayalalithaa Jayaram

Jayalalitha Haki miliki ya picha @AIADMK
Image caption Mwili wa Jayalalitha ukiwa umevikwa bendera ya India

Maelfu ya waombolezaji wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho kwa Jayalalithaa Jayaram, mmoja wa wanasiasa mashuhuri nchini India,.

Mkuu huyo wa serikali ya jimbo la Tamil Nadu alipatwa na mshtuko wa moyo Jumapili usiku na akafariki saa 23:30 (18:00 GMT) siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa hospitali ya Apollo, mjini Chennai.

Mwili wake, ukiwa umevikwa bendera ya India, umewekwa kwa ajali ya kutazamwa na umma katika ukumbi mkubwa katika makao makuu ya jimbo hilo.

Polisi wa ziada wametumwa kudhibiti waombolezaji na kushika doria huku kukiwa na wasiwasi wa kuzuka kwa fujo.

Alikuwa anaenziwa sana na wafuasi wake, baadhi ambao walikuwa wanamwita "Amma" (mama) na kuna wasiwasi kwamba huenda baadhi wakaamua kujidhuru au kuzua ghasia.

Awali, baada ya taarifa za kifo chake kutangazwa, kulitokea makabiliano kati ya polisi na wafuasi wake nje ya hospitali hiyo ya kibinafsi ya Apollo. Taarifa hizo baadaye ziliondolewa, ingawa saa chache baadaye alithibitishwa kufariki.

Baadhi ya wafuasi wake wamekuwa wakilia hadharani na kujipiga vichwa na vifuani.

Haki miliki ya picha @AIADMK
Image caption Maelfu ya watu wamejitokeza kutoa heshima zao za mwisho

Jimbo la Tamil Nadu limetangaza siku saba za maombolezi.

Serikali kuu mjini Delhi nayo imetangaza Jumanne kuwa siku ya mapumziko ya kitaifa kama heshima kwake.

Waziri Mkuu Narendra Modi atahudhuria ibada ya mazishi ya kiongozi huyo ambayo yatafanyika baadaye Jumanne.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kumekuwa na wasiwasi kwamba huenda wafuasi wake wakazua fujo
Haki miliki ya picha AP
Image caption Baadhi walikimbiza gari la kubeba wagonjwa lililobeba mwili wake
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Taarifa za kupotosha kuhusu kifo chake awali ziliwafanya wafuasi wake kulia kwa huzuni
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafuasi wa Jayalalitha wakiwa na picha yake
Haki miliki ya picha AP
Image caption Maafisa zaidi wa polisi wametumwa Chennai
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Msako wa polisi miaka ya 1990 uligundua sari 10,500 na jozi 750 za viatu nyumbani kwa Jayalalitha

Jayalalitha aliishi maisha yenye visa vingi, hadharani na faraghani.

Aliigiza katika zaidi ya filamu 100 kabla ya kujiingiza katika siasa.

Jayalalitha baadaye alichukua udhibiti wa chama cha AIADMK kutoka kwa mke wa mwanzilishi wa chama hicho, na kisha akashinda uchaguzi 1991.

Alikuwa ametuhumiwa kwa kujihusisha na ufisadi, na alikaa jela vipindi viwili vifupi, karibuni zaidi 2014.

Mahakama kuu mjini Karnataka ilimuondolea makosa mwaka 2015 na akarejea uongozini.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii