Wafanyakjzi wa misaada: Yemen hatarini kukumbwa na njaa

Yemen Haki miliki ya picha Atlas
Image caption Yemen

Yemen iko hatarini kukumbwa na baa la njaa hali iliyosababishwa na mzozo wa kisiasa uliokuwa ukiikabili nchi hiyo.

Afisa wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Jammie McGoldrick ameiambia BBC kwamba tayari kuna watoto walio fariki dunia kutokana na njaa.

Nalo shirika la Kimataifa la Oxfam limesema kwamba baada ya miaka miwili ya mapigano, Yemen imekuwa taratibu ikiangamizwa na baa hilo.

Shirika hilo limeutaka Muungano wa majeshi yanayoongozwa na Saudia, yanayopambana na waasi wa Ki Houthi, kuondoa vikwazo walivyoweka ambavyo vinazuia uingizwaji wa chakula.

Oxfam limeyataka pia mashirika ya wahisani kuongeza michango yao, katika kutoa huduma za kibinadamu.