Wanawake 100 Mwaka 2016: Ni kina nani waliosahaulika?

Huwezi kusikiliza tena
Wanawake 100: Kuongeza maelezo ya watu Wikipedia

Je, wajua wanawake ni asilimia 17% pekee ya watu mashuhuri ambao wasifu zao au maelezo kuwahusu yamo kwenye mtandao wa Wikipedia?

BBC, chini ya mradi wake wa makala za Wanawake 100, imeshirikiana na mashirika mengine pamoja na Wikipedia kuandaa shughuli ya siku zima tarehe 8 Desemba kujaribu kupunguza pengo hili la jinsia.

Shughuli hii itahusisha kuandika na kuhariri makala kuhusu wanawake katika mtandao wa Wikipedia.

Kutaandaliwa hafla 15 katika nchi 13 na kwa lugha mbalimbali, lengo likiwa kuongeza idadi ya wanawake wanaoweza kuhariri mtandao wa Wikipedia na pia kuongeza idadi ya wanawake ambao maelezo yao yamo kwenye mtandao huo.

Idhaa ya Kiswahili ya BBC itaandaa hafla ya kipekee jijini Nairobi kuanzia saa nne mchana.

Wanawake na wanaume watashiriki katika hafla hiyo, na unaweza kujiunga nao kwenye kompyuta yako.

Je, ungepewa nafasi ya kuongeza maelezo ya mwanamke fulani katika Wikipedia, ungemuongeza nani?

Tuandikie katika Twitter, Facebook na Instagram ukitumia kitambulisha mada #100WomenWiki.

Tazama video iliyo hapa juu ili kufahamu jinsi ya kufanya hivi.

Mada zinazohusiana