Maelfu wajitokeza kupiga kura Ghana

Usalama umeimarishwa kote Ghana
Image caption Maelfu wamejitokeza kupiga kura

Maelfu ya wapiga kura nchini Ghana wamepiga foleni, ndefu kwenye vituo vya kupigia kura kumchagua Rais na wabunge wapya katika Uchaguzi Mkuu wa leo.

Kuna ushindani mkali kati ya Rais John Mahama na mwanasiasa maarufu, Nana Akufo Addo.

Wagombea wote saba wa Urais wameahidi kuweka amani hususan wakati matokeo yakianza kutangazwa.

Jumatatu ya wiki hii mfuasi wa upinzani alifariki dunia wakati kulipozuka ghasia katika mkutano wa kampeini.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Rais John Mahama na Kiongozi wa Upinzani Nana Akufo-Addo

Mada kuu kwenye kampeini zimekua uchumi na Ufisadi.

Matokeo rasmi yanatarajiwa kutolewa katika kipindi cha siku tatu.

Ikiwa Rais John Mahama wa chama tawala cha 'National Democratic Congress'(NDC) atashindwa atakua kongozi wa kwanza Ghana kuhudumu kwa muhula mmoja pekee tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi vya kisiasa.

Rais huyo amekosolewa vikali kutokana na kukatizwa kwa huduma za umeme kila mara nchini.

Bwana Akufo-Addo ameahidi kuweka elimu ya bure ya sekondari na kujenga viwanda zaidi.

Huwezi kusikiliza tena
Raia wajitokeza kwa wingi kupiga kura Ghana

Wakosoaji wake wamesema hana mpango makhususi jinsi ya kuafikia mpango wake.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii