Sasa utaweza kufungia maoni Instagram

Instagram Haki miliki ya picha Instagram

Instagram wameboresha viungo vyao vya usalama kuwawezesha watu kufungia maoni ya watu kwenye picha na video wanazopakia.

Hii ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kuwezesha hilo.

Kampuni hiyo inasema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za "kuweka jukwaa hili likiwa salama na la kuvutia kila mtu".

Aidha, sasa itawezekana kwa mtu kuwaondoa watu wanaomfuata kwenye mtandao huo.

Mambo haya yaliwezekana kwa akaunti chache sana zilizokuwa zimeidhinishwa na kampuni hiyo.

Lakini sasa, hilo litatekelezwa kwenye akaunti ya kila mtu, katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Haki miliki ya picha Instagram

Awali, iwapo ulikuwa umemuidhinisha mtu kukufuata, hungeweza kumuondoa.

Lakini sasa hilo limekuwa rahisi sana.

Unaenda kwenye orodha ya watu wanaokufuata, unabofya palipo na alama '…' pembeni mwa jina la mtu.

Mtu huyo hatajulishwa kwamba umemuondoa au kumfungia.

Selena Gomez ndiye maarufu zaidi Instagram 2016

Kampuni hiyo imefichua kwamba mwanamuziki Selena Gomez ndiye maarufu zaidi katika Instagram, kando na akaunti ya Instagram yenyewe.

Maadui

Si wote wanaoipenda Instagram. Justin Bieber majuzi alisema Instagram ni "jehanamu" alipokuwa akitumbuiza London.

Alifuta akaunti yake mwezi Agosti baada ya mpenzi wake wa wakati huo Sofia Richie kumwagiwa matusi.

Kupenda maoni Instagram

Instagram pia wanaongeza kiungo cha kukuwezesha kupiga ripoti iwapo utaihisi rafiki yano anatafakari au yumo kwenye hatari ya kujidhuru.

Mtu huyo ataunganishwa na mashirika yanayotoa usaidizi au ushauri nasaha.

Aidha, utaweza kupenda maoni ambayo watu wametolea picha au video ulizopakia.

Mada zinazohusiana