Shambulio laua watu 63 ngome ya IS Iraq

Shambulio hilo lilitekelezwa kutoka angani Haki miliki ya picha AMAQ

Shambulio la anga lililofanywa katika mji wa Iraq unaoshikiliwa na wapiganaji wa Islamic state limeripotiwa kuua raia kadhaa.

Duru za afya kutoka katika mji wa Qaema karibu na mpaka wa Syria zinasema watu 63 wamekufa.

Taarifa za awali pia zinasema shambulio hilo lililenga kushambulia msikiti uliokuwa ukitumika kama makao makuu ya IS, lilikosea njia.

Kwa upande wake majeshi yanayoongozwa na Marekani pamoja na majeshi ya Iraq walifanya mashambulizi katika maeneo ya waasi hao.

Haijafahamika bado nani kati ya hao anawajibika kwa shambulio hilo.