Mji wa Mosul kukombolewa kwa wiki mbili

Wapiganaji wa kundi la IS
Image caption Wapiganaji wa kundi la IS

Kiongozi wa kikosi cha marekani nchini Iraq Generali Stephen Townsend amesema zinahitajika wiki mbili kuweza kuukomboa mji wa Mosul kutoka kwa wapiganaji wa kiislam (IS). Kikosi hicho kinasaidia wanajeshi wa iraq katika mapigano makali yanayoendelea kwa takribani wiki kadhaa. Generali Townsend amesema anaamini wapiganaji wakiislam wanafahamu wazi kuwa watapoteza miji yote wanayoishikilia,na kuhamishia maasi yao mafichoni. Kiongozi huyo pia amesema watashambulia nchi za magharibi mpaka watakapokamilisha kazi yao.