Michuano ya Europa ligi kuendelea leo

Man United Haki miliki ya picha AP
Image caption Wachezaji wa Manchester United wakifanya mazoezi kujianda na mchezo dhidi ya Zorya

Mshike mshike wa michuano ya Europa ligi utaendelea tena leo kwa michezo kumi na mbili kupigwa katika viwanja tofauti.

katika kundi A Mashetani wekundu wa Manchester united wako ugenini nchini Ukraine, kukipiga na Zorya Luhansk huku Feyenoord wakicheza na Fenerbahce.

Southampton watakua nyumbani katika dimba la St Marys kuwaalika Hapoel Be'er Sheva, FK Qarabag watakipiga na Fiorentina.

Sporting Braga wao watacheza na Shakhtar Donetsk, huku Villarreal wakipepeta na Steaua București .Apoel Nicosia wao watachuna na Olympiakos.

Waholanzi wa AZ Alkmaar watawalika Zenit St Petersburg ya nchini Urusi