Talaka tatu marufuku India

India
Image caption Kibonzo kinachoonesha furaha ya wanawake dhidi ya talaka

Mahakama moja kaskazini mwa India, imefutilia mbali utaratibu wa dini ya kiislamu wa talaka tatu ambao unampa nafasi mwanamume wa kiislam kumuacha mkewe kwa kusema mara tatu 'talaka' na kusema kwamba si utaratibu wa kisheria na ni kinyume cha katiba.

Mahakama kuu ya Allahabad imesema kwamba utaratibu huo umekuwa ukikiuka haki za wanawake wa kiislam .

Mahakama kuu nchini India kwa sasa inaendelea kusikiliza changamoto tofauti zinazotokana na utaratibu huo wa talaka.

Wakosoaji wa mambo wanasema marufuku hiyo inaweza kuwaondoa wanawake wa kiislam katika ufukara.Nchini India ,ndoa katika baadhi ya jamii hutumia sharia za kiislam na baadhi hufuata taratibu na sheria za serikali .

Wafuasi na wanaunga mkono utaratibu huo wa talaka tatu tayari wamesha toa tamko kuwa mjadala huo wa hivi karibuni umewalenga waislamu na kwamba ni kinyume cha haki.

Mjadala unaendela.