Mtandao wa tume ya uchaguzi Ghana wadukuliwa

Maelfu walijitokeza kupiga kura
Image caption Maelfu walijitokeza kupiga kura

Wadukuzi wa mitandao wamevamia mtandao wa tume ya uchaguzi nchini Ghana na kuuvuruga siku moja baada ya uchaguzi wa urais katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

Tume ya uchaguzi nchini Ghana inasema kuwa imelaani jaribio hilo la kuudukua mtandao wake.

Kwenye ukurasa wake wa Twitter tume hiyo ilisema kuwa taarifa inayodai kuwa mgombea wa upinzani Nana Akufo Addo alikuwa mbele ya rais wa sasa John Mahama ilikuwa ya uongo.

Image caption Mtandao wa tume ya uchaguzi unaonekana kukubwa na matatizo

Haijabainika ikiwa taarifa hiyo ilionekana kwenye mtandao wa tume ya uchaguzi, ambao kwa sasa unaonekana kukumbwa na matatizo.