Mbona Air Force One ni ghali mno?

Air Force One ikiingia Cuba mnamo Machi 20 mwaka 2016 Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Air Force One ikiingia Cuba mnamo Machi 20 mwaka 2016

Serikali ya Marekani inatarajiwa kutumia takriban dola bilioni 3.2 kwa maradi wa kuuunda ndege mpya ya Air Force One - jambo ambalo halijamfurahisha Donald Trump

Rais huyo mteule alisema kuwa ni wakati wa kufuta kandarasi ya kujenga ndege hiyo, ambayo kawaida hugharimu dola milioni 378.5 kwa ndege kawaida kama hiyo kwa mashirika ya ndege.

Lakini mbona ndege hiyo maarufu zaidi duniani ni ghali mno?

Namba moja

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Air Force One ikiwa kituo cha Joint Base Andrews huko Maryland tarehe 6 Disemba mwaka 2016

Air Force One, si ndege moja bali ni jinalinalopewa ndege maalum yenye sifa za kijeshi ambayo humbeba rais.

Ndege ya sasa, ilianza kutumiwa miaka ya tisini na muda wake wa kutumika unaelekea kikomo, kwa hivyo ndege nyingine aina ya Boeng 747 -8 imeagizwa na jeshi la Marekani

Ubabe wa kijeshi

Ukisema kuwa rais anasafiri kwa ndege ya 747-200 haileti picha kamili. Air Force One haswa ni iina ya ndege ya kijeshi ya VC-25A.

Muundo wake umechorwa kwa njia maalum na kuiwezesha ndege hiyo kuwa kama makao ya rais ikiwa Marekani itashambuliwa

Haki miliki ya picha AP
Image caption Ndege ambayo inatachukua mahala pa ndege ya sasa huenda ikawa kubwa zaidi

Bajeti ya ndege hiyo inajumuishwa kuundwa kwa njia maalum na kuboresha mifumo yake ya eletroniki kwa mfano.

Ndege ya Air Force One imeunda kwa njia ambayo ina uwezo wa kuzuia athari zozote za shambulizi zinazoweza kuharibu mifumo yake ya eletroniki kama vile kulipuliwa kwa bomu la nyuklia angani.

Ndege hiyo pia huwekewa vifaa vya mawasiliano ya kijeshi na vifaa vya kujikinga yenyewe.

Hii inamaanisha kuwa Air Force One ina uwezo ya kuzuia makombora.

Huwezi kusikiliza tena
Je ndege ya Air force One inaonekanaje?

Hatua ya kwanza ya kupata ndege ya aina hii ni kwa kuagiza ndege mbili aina ya 747-8 za abiria - ndipo shughuli ya kuanza kuundwa kwao kwa njia maalum huanza.

Ndege mbili uhitajika, licha na rais kuwa mmoja, ili kuhakisjha kuwa wakati ndege moja inafanyiwa ukarabati, ya pili iko tayari kutumika.

Ndege ya Trump na Air Force One gani bora zaidi?

Wakati moja wa mahojiano, bwana Trump alidai kuwa ndege yake binafsi ni kubwa kuliko Air Force One.

Hilo si kweli.

Ndege ya Trump ya Boeing 757-200 ni ndogo kwa kila njia kuliko Air Force One. Kulingana na kampuni ya Boeng, Air Force One ina urefu wa futi 231 na nukta10 au mita 70,6 huku mabawa yake yakiwa na urefu wa futi 195 au miata 59.6.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndege ya Trump ya 757 ni ya kifahari lakini ndogo kuliko Air Force One

Ndege ya bwana Trump ina urefu wa futi 155 au mita 47 na mabawa yake yana urefu wa futi 134 au mita 40

Pia Air Force One inaishinda ndege ya Trump kwa nguvu.

Ina uwezo wa kusafiri mbali kuliko ndege zingine, ikiwa na uwezo wa kusafiri kutoka Washington hadi Hong Kong kwa safari moja. Pia ina uwezo wa kuongezwa mafuta ikiwa hewani.

Ndege ya Air Force One ina sehemu mbili za kupika chakula cha kuweza kuwalisha watu 100 kwa wakati mmoja, Chakula hupikwa na wapishi wa kijeseshi.

Image caption Air Force One

Gharama ya juu

Gharama ya kufanikisha huduma za ndege ya Air Force One ni kati ya dola 180,000 na doa 200,000 kwa makadirio.

Hilo ni suala ambalo Trump analipinga vikali.

Ikiwa Trump anataka kupunguza gharama yake ya kusafiri , atahitajika kuanza na kuzua kununuliwa kwa ndege ya aina hii.