Blatter amlaumu Infantino kwa kutopokea simu zake

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Blatter amlaumu Infantino kwa kutopokea simu zake

Aliyekuwa rais wa shirikishjo la kandanda duniani Fifa, amemlaumu mrithi wake Gianni Infantino kwa kutomheshimu akisema kuwa rais huyo mpya wa Fifa hapokei simu zake.

Blatter mwenye umri wa miaka 80 anasema alikutana na Infantino kujadili masuala ambayo yanaweza kusuluhishwa kwenye shirikisho la Fifa.

"Infantino akasema, nitalishughulikia hilo, na hakuwezi kurudi tena," amesema Blatter.

Marufuku ya miaka sita aliyopewa Blatter kutoka kwa shughuli zozote za kandanda ilifutwa wiki hii baada ya kukatwa rufaa.

"Sijaona kwenye kampuni yoyote ambapo rais mpya haonyeshu heshima kwa mtangulizi wake," alisema Blatter wakati wa mahojiano na BBC.

"Baada ya kuchaguliwa kwake, tulikuwa na mawasiliano mazuri na alikuja hata kwangu na tukafanya mazungumzo. Nikamuambia kuwa nina maswali kadha ambayo yanahitajika kutatuliwa katika Fifa."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Blatter alitimuliwa kutoka Fifa baada ya kupatikana kulipa pauni milioni 1.3 kwa aliyekua mkuu wa Uefa Michel Platini.

Nimemuuliza, nimemtumia barua na nina namba yake na niliambiwa bado iko sahihi, hawezi kupokea simu, hawezi, alisema Blatter.

Blatter alitimuliwa kutoka Fifa baada ya kupatikana kulipa pauni milioni 1.3 kwa aliyekua mkuu wa Uefa Michel Platini.

Wote walitimuliwa na Fifa kwa miaka minne mwezi Disemba, lakini marufuku hiyo ikapunguzwa hadi miaka sita.