Grace Mugabe katika mzozo wa pete ghali ya almasi

Grace Mugabe Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Grace Mugabe

Gazeti la Zimbawe Independent la nchini Zimbabwe, leo hii limechapisha ripoti kuwa mke wa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe, Grace Mugabe anashtakiwa kutokana agizo aliloweka kwa pete ghali zaidi ya almasi.

Taarifa hiyo inaendelea kusema kuwa Bi Mugabe alikuwa amesema kuwa mmewe alikuwa anataka kununua pete hiyo kuadhimisha miaka 20 ya ndoa yao.

Pete hiyo iliagizwa kutoka kwa muuzaji mjini Dubai kutoka kupitia kwa mfanyibiashara mmoja.

Kesi hiyo inaonekana kuwa ngumu na ina madai yanayohusu mmoja wa wanawe wa kiume na mlinzi wake.