Vituo vya radio vyadai "ushindi" kwa upinzani Ghana

Wafuasi wa Akufo-Addo wakishangilia baada ya madai kutangazwa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wafuasi wa Akufo-Addo wakishangilia baada ya madai kutangazwa

Vituo viwili vya Radio nchini Ghana vimekuwa vikiripoti kuwa kiongozi wa upinzani Nana Akufo-Addo ameshinda uchaguzi wa urais licha ya kutotangazwa kwa matokeo rasmi.

Bwana Akufo-Addo amekosolewa na mukundi ya waangalizi wa kura, kwa kudai ushindi wakati matokeo ya kura yakiwa yanasubiriwa kwa hamu.

Akufo-Addo alikuwa amesema kuwa ana uhakika alikuwa ameshinda rais John Mahama.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption John Mahama (kushoto) na Akufo-Addo (kulia)

Hata hivyo afisa kutoka upande wa Mahama alitupilia mbalia madai hayo.

Vituo vya Radio vya Joy FM na Citi FM, vimeyasema hayo kuambatana na matokeo yaliyotangazwa katika maeneo bunge.

Joy FM ilisema kwa bwana Akufo-Addo alikuwa na asilimia 53huku bwana Mahama akiwa na asilimia 45 kutokana na kuhesabiwa kura katika maeneo bunge 217 kati ya maeneo 275.

Radis ya Citi nayo ilimpa Akufo-Addo asilimia 55 kwenye maeneo bunge 190.