Wanasiasa wa upinzani Burundi wamkataa Mkapa

Mkapa amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.
Image caption Mkapa amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.

Wanasiasa wa upinzani nchini Burundi walio uhamishoni wamepinga jitihada za aliyekuwa rais wa Tanzania za kutatua mzozo ulio nchini humo.

Hii inajiri baada ya William Mkapa kuwaambia waandishi wa habari kuwa si jambo zuri kuendelea kutilia shaka uhalali wa Raia Pierre Nkurunzia.

Nchi ya Buurndi ilitumbukia kwenye mzoo baada ya bwana Nkurunziza kutangaza kuwa angewania muhula wa tatu.

Mamia ya watu wameuawa na maelfu kukimbia nchi kulipozuka ghasia.

Bwana Mkapa alipewa jukumu la kusaidia kutatua mzozo huo, na amesema kuwa makubaliano yataafikiwa ifikapo mwezi Juni mwaka ujao.

Baadhi ya wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni wanatafutwa na serikali kwa kupanga maandamano ya kupinga hatua ya Rais Nkurunziza hatua ambazo serikali inazitaja kuwa za kihalifu.

Wengine waliilaumiwa wa kushiriki kwenye mapinduzi ya kijeshi yaliyofeli mwezi Mei.