Mlipuko mkubwa wakumba eneo la bandari ya Mogadishu Somalia

Watu 16 wauawa Somalia
Image caption Watu 16 wauawa Somalia

Maafisa wakuu nchini Somalia wanasema kuwa mlipuko mmoja wa bomu ambalo lilikuwa limetegwa ndani ya gari, umelipuka na kuwauwa watu 16 karibu na mji mkuu ulioko bandarini mwa Mogadishu.

Kuna taarifa kuwa huenda watu wengi zaidi wamefariki kuliko idadi iliyotolewa.

Walioshuhudia wamesema kuwa mshambuliaji alikuwa ni wa kujitoa mhanga.

Mara baada ya mlipuko huo, milio ya risasi ilifuatia.

Kundi la wapiganaji wa Taliban limekiri kutekeleza mauaji hayo.