Trump akana madai kuwa Urusi ilishawishi uchaguzi

Trump akana madai kuwa Urusi ilishawishi uchaguzi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Trump akana madai kuwa Urusi ilishawishi uchaguzi

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema haaminiakuwa ripoti ya CIA ambayo ilisema kuwa wadukuzi wa Urusi walijaribu kushawishi matokeo ya uchaguzi wa Marekani kwa kumpendelea.

Katika mahojiano na kitoa cha Fox News, Trump aliwalaumu wanademokratic kwa taarifa hizo zinazosema kuwa Urusi ndiyo iliendesha udukuzi huo.

Maafisa wa Urusi mara nyingi wamekana madai hayo.

Maafisa wa vyeo vya juu katika Republican sasa wamejiunga na wenzao wa Democratic wakitaka mashirika ya ujasusi kufanyiwa uchunguzi.

Kwa taarifa ya pamoja Seneta wa Republican John MacCain na seneta wa Democratic Chuck Schhumer wamesema kuwa kuwa ripoti ya CIA ni kumweka wasi wasi kila mmarekani.