Boko Haram: Watoto watekeleza shambulio sokoni Nigeria

Eneo la shambulio Maiduguri. 11 Desemba 2016 Haki miliki ya picha AFP

Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa wasichana wawili wamelipua mabomu mawili katika soko lililoko kwenye jimbo la Borno na kumuua takriban mtu mmoja.

Mwanamgambo mmoja katika mji wa Maiduguri amesema kuwa watoto wasichana hao ambao pia waliuawa walikuwa na umri wa miaka saba na minane.

Alisema kuwa aliwaona wakitoka nje ya Bajaji na kujaribu kuzungumza na mmoja wao, ambaye baadae alielekea kwenye jengo lenye maduka mengi na kulipua vilipuzi.

Hakuna aliedai kuhusika na shambulio hilo, lakini waandishi wa BBC wanasema kundi la Boko Haram mara kwa mara hutumia wanawake na watoto katika mashambulio yake ya mabomu.

Image caption Watoto wasichana waliotekeleza shambulio walikuwa na umri wa miaka saba na minane

Mada zinazohusiana