Putin akataa zawadi ya mbwa kutoka Japan

Vladimir Putin na mbwa wake 2013 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mbwa huyo alitarajiwa kuwa 'mpenzi' wa Yume (kushoto), ambaye alikabidhiwa Bw Putin kama zawadi mwaka 2012. Kulia ni mbwa kwa jina Buffy

Rais wa Urusi Vladimir Putin amekataa zawadi ya mbwa aina ya Akita kutoka kwa serikali ya Japan, mbunge mmoja nchini Japan amesema.

Koichi Hagiuda hakueleza sababu ya zawadi hiyo kukataliwa.

Japan ilimpa Putin mbwa jike kwa jina Yume, pia wa aina ya Akita, mwaka 2012.

Mbwa huyo mpya alifaa kuishi na Yume.

Bw Hagiuda ameandika kwenye blogu: "Inasikitisha, tumesikia kutoka kwa washirika wetu, na matumaini yetu ya kuwasilisha bwana harusi yamevunjwa."

Mpango ulikuwa kwamba Bw Putin angepewa mbwa huyo na Waziri Mkuu wa Japan Shinzo Abe akiwa ziarani Japan wiki ijayo.

Mbwa aina ya Akita wana asili yao kaskazini mwa Japan.

Bw Putin kwa sasa anamiliki mbwa dume aina ya Bulgarian Shepherd ambaye huitwa Buffy.

Alipewa mbwa huyo kama zawadi na waziri mkuu wa Bulgaria mwaka 2010.

Ana pia mbwa mwingine aina ya Labrador kwa jina Konni, zawadi kutoka kwa Sergey Shoigu, waziri wa ulinzi wa Urusi aliyefariki 2014.

Bw Putin wakati mmoja aliandamana na Konni kwenye mkutano na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, ambaye huwaogopa sana mbwa.

Baadhi ya taarifa kwenye vyombo vya habari zilisema Bw Putin hakufahamu kwamba Merkel anaogopa sana mbwa.

Alisema: "Nilipofahamu kwamba hawapendi mbwa, niliomba radhi, bila shaka."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii