Ajali iliyowaua zaidi ya watu 33 Kenya

Ajali iliyowaua zaidi ya watu 30 Naivasha, Kenya
Image caption Ajali iliyowaua zaidi ya watu 30 Naivasha, Kenya

Siku ya Jumamosi usiku gari linaloaminika kubeba kemikali ambayo inashika moto kwa haraka, lililokuwa safarini kutoka mjini Mombasa kwenda Kampala Uganda, lilihusika kwenye ajali mbaya karibu na mji wa Naivasha ulio Kaskazini Magharibu mwa mji mkuu wa Kenya Nairobi.

Jumla ya watu 33 waliangamia, wengi miili yao ikichomeka hadi kutoweza kutambuliwa, na wengine kadha wakipata majeraha.

Taarifa zinasema kwa gari hilo lenye nambari za usajili za Uganda lililokuwa limebeba kemikali liligonga tuta katika eneo la Karai karibu na Naivasha mwendo wa saa tatu unusu usiku wakati ambapo watu wa eneo hilo walikuwa wakifunga biashara zao.

Baada ya kugonga tuta la barabarani gari hilo lilipoteza mwelekeo na likagonga magari mengine yaliyokuwa barabara wakati huo likiwemo lililokuwa na na maafisa 11 wa polisi wa kumlinda rais na kisha likalipuka na kushika moto.

Image caption Ajali iliyowaua zaidi ya watu 30 Naivasha, Kenya

Jumla la magari 13 yalishika mto na karibu watu wote waliokuwa ndani ya magari hayo wakaangamia.

Walioshuhudia walisema kuwa moto huo ulisambaa kwa haraka huku watu wengine wakijaribu kujiokoa bila ya kufanikiwa.

Wengi waliofika kujionea ajali hiyo walisema kuwa kamwe hawangestahimili kuona kwa macho yao jinsi watu waliteketea na hali mbaya ambayo maiti hizo zilikuwa.

Inaarifiwa kuwa gari la wazima moto lilichelewa kufika eneo la ajali kutokana na msongamano wa magari uliosababishwa na ajali hiyo

Eneo la Karai kwa muda mrefu limeshuhudia ajali mbaya za barabarani.

Wenyeji wa eneo hilo wanasema kwa waliomba matuta kuwekwa eneo kutokana na visa vingi vya ajali vilivyokuwa vikitokea kila mara.

Mkaazi mmoja alinukuliwa akisema kuwa zaidi ya watu 10 walikuwa wakiuawa eneo hilo kila mwezi kwa kugonjwa na magari barabarani au kwa njia zingine.

Image caption Ajali iliyowaua zaidi ya watu 30 Naivasha, Kenya

Ajali hii ingeweza kuepukika?

Matuta yaliwekwa ili kulazimisha magari kupunguza mwendo.

Hata hivyo kuwepo kwa matuta hayo barabarani kumekosolewa na watu wengine, wengine wakidai kuwa matuta hayo yaliweka bila ya kuwepo ishara za kunyesha kuwa yapo.

Hii ni sababu kuwa mara nyingi gari likigonga tuta kwa ghafla linaweza kupoteza mwelekeo na kusababisha ajali.

Image caption Ajali iliyowaua zaidi ya watu 30 Naivasha, Kenya

Ni bayana kuwa ikiwa kungekuwa na dalili za kuonyesha kuwa matuta yako barabarani huenda ajali kama hii haingetokea kuwa kuwa labda dereva wa lori lililokuwa limebeba kemikali, angekuwa mwangalifu asije akaligonga tuta kwa ghafla.

Akithibitisha ajali hiyo, waziri wa masuala ya ndani nchini Kenya Joseph Nkaissery alisema kuwa ni watu 33 waliaga dunia wakimemo polisi 11 wa kikosi cha Recce ambacho humlinda rais na watu wengine mashuhuri.

Waziri Nkaisssery pia alisema kuwa sio gari la kusafirisha mafuta lililolipuka bali gari aina ya Canter lililokuwa na mitungi ya kemikali inayoshika moto kwa haraka, iliyokuwa ikisafirishwa kutoka Mombasa kwenda Kampala, Uganda.

Image caption Ajali iliyowaua zaidi ya watu 30 Naivasha, Kenya

Akihutubia taifa wakati wa shere za maadhimisho ya siku ambapo Kenya ilitangazwa kuwa Jamhuri, Rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa hatua ya kuweka matuta eneo hilo bila ya kuwepo ishara za kutoa tahadhari yalikuwa ni makosa.