Muungano wa upinzani wamtaka Jammeh aondoke madarakani

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Yahya Jammeh

Muungano unoongozwa na rais mteule wa Gambia Adama Barrow, umemtaka kiongozi wa miaka mingi wa nchi hiyo Yahya Jammeh, aondoke madarakani na kukabithi mamlaka.

"Nafikiri anastahili kuondoka madarakani. Ameshindwa kwenye uchaguzi, hatutaki kupoteza wakati, tuna taka nchi hii iendelee mbele." Barrow alinukuliwa na shirika la AFP.

Bwana Jammeh amesema kuwa ana mipango ya kupinga matokeo hayo katika mahakama ya juu, baada ya kubadilisha mawazo siku ya Ijumaa baada ya kutangaza kukubali kushindwa awali.

Gambia kwa sasa haina mahakama ya juu inayohudumu na muungano wa upinzani unasema kuwa Rais hana mamlaka kikatiba katika siku zake za mwisho madarakani kuwateua majaji wapya kusikiliza kesi hiyo.