Viongozi kadha kuwasili Gambia kumshawishi Jammeh

Jammeh anataka uchaguzi mpya kufanyika Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jammeh anataka uchaguzi mpya kufanyika

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajiwa kuwasili nchini Gambia leo hii katika jaribio la kumshawishi rais wa Gambia Yahya Jammeh kuondoka madarakani baada ya kushindwa kwenye uchaguzi mkuu.

Bwana Buhari anatarajiwa kujiunga na rais wa Liberia Ellen Johnson-Sirleaf, rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma na rais wa Ghana John Mahama ambaye mwenyewe alishindwa kwenye uchaguzi wiki iliyopita na ambaye tayari amesema kuwa ataondoka madarakani mwezi ujao.

Baada ya kukubali kushindwa mwishoni mwa wiki iliyopita, alitangaza baadaye kuwa hakubaliani na matokeo na kutaka kufanyika kwa uchaguzi mpya,

Rais mteule Adama Barrow amekaribisha mipango ya ziara ya viongozi hao na inaripotiw kuwa yeye pia atakutana nao.

Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Gambia alimtangaza mgombea wa upinzani Adama Barrow, kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa mwaka huu.

Adama Barrow alipata kura 263,515 huku Rais Yahya Jammeh akipata kura 212,099.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii