Trump amteua Rex Tillerson waziri wa mambo ya nje

Rex Tillerson Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rex Tillerson

Rais mteule nchini Marekani Donald Trump amethibitisha kuwa mkuu wa kampuni ya Exxon Mobil, Rex Tillerson ndiye waziri wa mambo ya nje nchini Marekani.

Bwana Trump alimsifu Tillerson mwenye umri wa miaka 64 kama mmoja wa viongoziwa biashara wenye tajriba kubwa zaidi duniani.

Bwana Tillerson anatajwa kuwa na uhusiano mwema na rais wa Urusi Vladimir Putin jambo ambalo limewatia wasiwasi wa wanademocrat na baadhi ya warepublican

Trump ajikita kuboresha uchumi Marekani

Trump akana madai kuwa Urusi ilishawishi uchaguzi

Uteuzi huo unahitaji kuthibitishwa na bunge la Senate.

Siku chache zilizopita ilibainika kuwa majasusi nchini Marekani wanaamini kuwa Urusi ilihusika na kushawishi ushindi wa Trump.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani ndiye mwanadiplomasia wa cheo cha juu zaidi ambaye uhusika na sera za kigeni za nchi.