Syria: Mapigano yaisha Mashariki mwa Aleppo

Maisha baada ya vita
Image caption Maisha baada ya vita

Operesheni za kijeshi zimemalizika mashariki mwa mji wa Aleppo, Balozi wa Urusi ndani ya Umoja wa Mataifa , ameeleza.

Vitaly Churkin amesema Serikali imeweza kudhibiti maeneo yaliyokuwa yamebaki mikononi mwa waasi.

Tangazo hilo kama litathibishwa, litakuwa limemaliza mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miaka minne.

Awali, bwana Churkin alisema mipango inapangwa ili kuwaondoa waasi kwenye mji huo, Waasi wameridhia mpango wa kuondoka.

Image caption Vita hivyo vilivyodumu kwa miaka minne vimeacha makovu makubwa

Makubaliano hayo yamekuja wakati ambao Umoja wa mataifa ukitoa ripoti ya mauaji yaliyotekelezwa na vikosi vya serikali ya Syria.

Ofisi ya umoja wa mataifa inayoshughulikia masuala ya haki za binaadam imesema ina ushahidi wa kuaminika kuwa katika maeneo manne raia 82 waliuawa, na kuongeza kuwa watu zaidi wameuawa.