Putin ataka kuonana na Trump baada ya kuingia madarakani

Wakati wa kampeni, Trump (kushoto) alionekaa kumuunga mkono Rais Putin
Image caption Wakati wa kampeni, Trump (kushoto) alionekaa kumuunga mkono Rais Putin

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema ataonana na Rais mteule wa Marekani Donald Trump mara tu atakapo apishwa kuingia madarakani.

Putin amewaambia waandishi wa habari kuwa alimuunga mkono Trump ili kuweka sawa uhusiano wa Marekani na nchi yake.

Putin ameongeza kuwa halitakuwa jambo rahisi ukizingatia na namna nchi zote mbili zinavyotofautiana kimisimamo, lakini atafanya kila awezalo kuweka mambo sawa zaidi.

Juma lililopita, Shirika la upelelezi nchini Marekani CIA liliishutumu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani kwa kumuunga mkono Trump.

Mada zinazohusiana