Mwanzilishi wa Jamii Forums azuiliwa Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Mwanzilishi wa Jamii Forums Maxence Melo azuiliwa Tanzania

Mwanzilishi wa mtandao maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wa Jamii Forums Maxence Melo anashikiliwa na polisi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Jamii Forums Melo anashikiliwa kwa kukataa kutoa taarifa za watumiaji wa mtandao huo.

Alitarijiwa kufikishwa mahakamani Jumatano asubuhi lakini wakili wake ameambia BBC hilo halikufanyika.

Badala yake, taarifa zinadokeza huenda akafikishwa kortini Jumanne asubuhi.

Wakili wa Bw Melo anatafakari uwezekano wa kuwasilisha ombi kortini kupinga kuzuiliwa kwa mteja wake kwa zaidi ya saa 24 bila kufikishwa kortini.

Awali, Mwandishi wetu Sammy Awami alizingumza na mwanzilishi mwenza wa Jamii Forums Mike Mushi na alianza kwa kuelezea mwanzo wa kesi hiyo.

Mada zinazohusiana