Kijana aliyepanga kumuua Trump afungwa

Sandford alikamatwa wakati wa mkutano wa Las Vegas Haki miliki ya picha AP
Image caption Sandford alikamatwa wakati wa mkutano wa Las Vegas

Mwanamme mmoja raia wa Uingereza amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela kufuatia jaribio lake la kutaka kunyakua bunduki kwa lengo la kumuua Donald Trump.

Michael Sandfgord mwenye umri wa miaka 20 alikiri makosa hayo ya kumiliki bunduki na kuvurua mkutano.

Analaumiwa kwa kujaribu kunyakua bunduki kutoka kwa polisis wakati wa mkutano wa hadhara huko Las Vegas ili kumfyatulia risasi mgombea urais.

Mahakama ilisema kuwa huenda akaachiliwa baada ya miezi minne ambapo atasafirishwa hadi nchini Uingereza

Baada ya Sandford kukamatwa aliwaambia maafisa kuwa alikuwa na mpango wa kumpiga risasi Donald Trump.

Hata hivyo hakufanikiwa kunyakua bunduki kutoka kwa afisa wa polisi.

Mamake alisema kuwa alikuwa amepoteza mawasiliano na mwanawe, ambaye aliondoka nyumbani kutembea kote marekani mwaka 2015.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Michael Sandford, akiwa na mamake

Kulingana na nyaraka za mahakama Sandfords ambaye hakuwa na makao na ambaye alikuwa akiishi Marakani kinyume na sheria baada ya muda wa visa yake kuisha, aliiwaambia majasusi kuwa aliendesha gari kutoka California hadi Nevada kwa lengo la kumpiga risasi Trump.

Anaripotiwa kumuambi afisa wa polisi kuwa alitarajia kuuawa kwenye shambulizi hilo na kwamba alikuwa na tikiti za kuhudhuria mkutano mwingine wa Trump baadaye ikiwa angapata fursa ya pili.

Majaji walitaja kitendo hicho kuwa cha kustaajabisha.