Mapigano makali yazuia watu kuondoka Aleppo

Mabasi yaliletwa lakini hayajatumika Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabasi yaliletwa lakini hayajatumika

Makubaliano ya kuwaondoa waasi na raia kutoka mashariki mwa Allepo nchini Syria, yanaonekana kugonga mwamba kufuatia kuwepo mashambulizi makubwa mjini humo.

Usitishwaji mapigano ulitangazwa mjini Aleppo siku ya Jumanne na mabasi kupelekwa ili kuwasafirisha watu kutoka mji huo ulioharibiwa.

Lakini mapigano yalirejea aena siku ya Jumatano. Wanaharakati nchini Syria wanasema kuwa mashambulizi ya angani katika enep linalodhibitiwa na waasi yamerejea.

Eneo la mashariki mwa mji wa Aleppo limedhibitiwa na waasi tangu mwaka 2012. Lakini sasa wamesukumwa kwenda eneo dogo miezi ya hivi karibuni na mashambulizi makubwa yanayofanywa na serikali ikisaidiwa na ndege za Urusi.

Siku ya Jumanne balozi wa Urusi kwenye umoja wa mataifa Vitaly Churkin alikiambia kikao cha baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuwa haratakati za kijeshi Mashariki mwa Aleppo zimekamilika.

Chini ya makubaliano ya kuondoka, raia na waasi kutoka mashariki mwa Aleppo wangeruhusiwa kueleka maeneo yanayodhitiwa na waasi mashariki mwa Syria.

Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Urusis Sergei Lavrov, anasema anataraji kuwa waasi watasalimu amri katika muda wa siku mbili au tatu zinazokuja.

Wenyeji walioakwama mashariki mwa Allepo wamekumbwa na mashambulizi ya wiki kadjha na uhaba mkubwa wa chakula. Vituo vya kutoa huduma za afya navyo vimeharibiwa eneo hilo.

Image caption Waasi wangeruhusiwa kueleka maeneo yanayodhitiwa na waasi mashariki mwa Syria