UN: Huenda Sudan Kusini ikakumbwa na mauaji ya kimbari

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Watu nchini Sudan Kusini wanajaribu kubaini ikiwa jamaa zao wamekufa au wako hai

Jamii ya kimataifa inaweza kuzuia mauaji ya kimbari sawa na yaliyoshuhudiwa nchini Rwanda yasitokee nchini Sudan kusini, ikiwa itatuma mara moja vikosi 4000 kote nchini humo na kubuni mahakama ya kuwashtaki wale ambao wemeendesha dhuluma, kwa amujibu wa mkuu wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa.

Akiongea kwenye mkutano maalmu wa baraza hilo mjini Geneva, Yasmin Sooka alisema kuwa Sudan Kusini, iko katika hatari ya kutumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo vitaathiri kanda nzima.

Sudan Kusini, amablo ni taifa janga zaidi duniani limekumbwa na mzozo tangu mwezi Disemba mwaka 2013, baada ya rais Salva Kiir kumlaumu makamu wakae aliyefutwa kazi Riek Machar kwa kupanga mapinduzi, madai ambayo Machar ameyakana.