Serikali ya Syria yaendelea kudhibiti maeneo muhimu ya Aleppo

Kuwekwa kwa bendera kunamaanisha udhibiti kamili wa Serikali ya Syria eneo hili
Image caption Kuwekwa kwa bendera kunamaanisha udhibiti kamili wa Serikali ya Syria eneo hili

Vikosi vinavyounga mkono serikali ya Syria vimeendelea kuchukua maeneo mengi Kaskazini mwa Aleppo baada ya kuisha kwa mapigano siku ya Jumanne.

Jeshi la Urusi limesema kwa sasa waasi wanashikilia maeneo machache sana ya mji huo yasilozidi kilometa mbili.

Uturuki na Urusi ambazo zilisaidia kwa pamoja kuwaondoa waasi zimesema usalama kamili utarejea siku za karibuni.

Iran ambayo pia inaunga mkono serikali ya Assad imesema makubaliano yoyote ni lazima yawahusu wananchi ambao bado wapo katika maeneo yanayozingirwa na waasi.

Mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi yamedumu kwa miaka minne.