Wabunge Austria waidhinisha nyumba ya Hitler itwaliwe

Hitler alizaliwa Braunau am Inn, Austria Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mmiliki wa sasa wa nyumba hiyo atalipwa fidia

Bunge nchini Austria limepitisha sheria inayotoa fursa ya kutwaa nyumba ambapo kiongozi wa zamani wa Ujerumani Adolf Hitler alizaliwa mwaka 1889.

Mmiliki wa sasa wa nyumba hiyo Gerlinde Pommer amekataa mara nyingi kuuza nyumba hiyo inayopatikana Braunau am Inn.

Amekataa pia kukubali ifanyiwe ukarabati.

Bi Pommer sasa atalipwa fidia na nyumba yake itwaliwe.

Lakini haijabainika serikali itafanyia nini nyumba hiyo ambayo zamani ilitumiwa kama mgahawa.

Serikali hata hivyo imeonyesha nia ya kutaka kuzuia nyumba hiyo kuwa kivutio kwa watu wanaofuata sera za Wanazi.

Uamuzi huo wa bunge utafikisha kikomo mzozo wa muda mrefu kati ya serikali na Bi Pommer, ambaye kwa sasa amestaafu.

Kwa miaka minig, serikali ilimlipa Bi Pommer kodi ya juu kumzuia asiruhusu jumba hilo la ghorofa tatu kugeuzwa na kuwa kama kivutio cha kitalii kwa Wanazi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Hitler alizaliwa katika chumba cha kukodishwa ghorofa ya juu ya jumba hilo

Zamani, jumba hilo lilitumiwa na shirika moja la kuwasaidia wasiojiweza kama kituo cha mafunzo na warsha kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum.

Lakini shirika hilo lililazimika kuhama miaka kadha iliyopita baada ya Bi Pommer kuzuia ukarabati ufanywe.

Kumwekuwa na mjadala kuhusu hatima ya jumba hilo, baadhi wakitaka libomolewe na wengine wakitaka matumizi yake yabadilishwe.

Wanahistoria hata hivyo wanasema kwa kulibomoa, watu watakuwa wameinyima Australia historia ya Nazi.

Hitler alizaliwa katika chumba cha kukodishwa ghorofa ya juu ya jumba hilo karibu na mpaka wa Austria na Ujerumani tarehe 20 Aptili Ujerumani.

Wakati wa utawala wa Nazi, liligeuzwa na kuwa madhabahu ambapo lilivutia watalii wengi.

Nazi walipoanza kushindwa na kupoteza udhibiti 1944, lilifungwa.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii