Wakenya hutaka kujua nini mtandaoni?

Wakenya wengi wanataka kujua "jinsi ya kupunguza unene haraka"
Image caption Wakenya wengi wanataka kujua "jinsi ya kupunguza unene haraka"

Mtandao wa Google umetoa ripoti inayobaini kwa undani upekuzi na maswali ambayo Wakenya waliuliza mtandaoni mwaka 2016.

Katika kitengo cha maswali yanayoanza na 'jinsi ya', "jinsi ya kupunguza unene haraka" liliulizwa na Wakenya wengi zaidi.

"Jinsi ya kulainisha nywele asili" lilikuwa swali la tatu kwenye orodha. Maswali mengine yaliyoulizwa ni "Jinsi ya kufanya ngozi iwe nyeupe kitaalamu", "jinsi ya kutongoza wasichana", "jinsi ya kupata tumbo bapa" miongoni mwa mengine.

Wakenya wengi walitafuta maelezo kuhusu afya yao. Maswali yaliyoongoza ni "jinsi ya kupunguza unene haraka" na "jinsi ya kupata tumbo bapa" .

"Jinsi ya kuhesabu siku za ujauzito," lilikuwa la tatu.

Maswala mengine ya kiafya yaliyotafutwa na Wakenya ni "jinsi ya kuzuia uvundo wa miguu" , "jinsi ya kupunguza msukumo wa damu", "jinsi ya kuhesabu siku salama za kushiriki ngono bila kupata mimba" "jinsi ya kuwa mnene kwa siku moja".

Wakenya pia walitaka kujua "Nini kinachotokea Aleppo". Wengi walitaka kujua hali ilivyo katika mji wa Aleppo uliokumbwa na mapigano makali kati ya wapiganaji na vikosi vya serikali.

Wakenya pia walitaka kujua "Nini kinachotokea Ethiopia?"

Hii inafuatia maandamano ya jamii za Amhara na Oromia nchini Ethiopia, ambayo yamesababisha mauaji ya takriban watu 100.

Maswala yaliyotafutwa sana.

1. Euro 2016

2. Donald Trump

3. Michezo ya Olimpiki 2016

4. Jacob Juma

5. Muhammad Ali

6. Hillary Clinton

7. Diana Chelele

8. Lucy Kibaki

9. Project X

10. Achieng Abura

Haki miliki ya picha Achieng Abura / Facebook
Image caption Achieng Abura alifariki dunia Oktoba

Matukio yaliyotafutwa na wakenya wengi

1. Michezo ya Olimpiki 2016

2. Uchaguzi wa Marekani

3. Brexit

4. UEFA Euro 2016

5. Uchaguzi wa Uganda

6. Tamasha la Holi

7. Uchaguzi mdogo wa Kericho

8. Harusi ya Bob Collymore

9. Ramadan 2016

10. Mkasa wa Huruma

Utafutaji unaoanza na "jinsi ya"

1. Jinsi ya kupunguza unene haraka

2. Jinsi ya kutengeneza blogu

3. Jinsi ya kulainisha nywele asili

4. Jinsi ya kuhifadhi pesa

5. Jinsi ya kufanya ngozi iwe nyeupe kitaalam

6. Jinsi ya kutongoza wasichana

7. Jinsi ya kupata tumbo bapa

8. Jinsi ya kutibu jereha la moto nyumbani

9. Jinsi ya kujibu maswali katika mahojiano ya kazi

10. Jinsi ya kuremba nyumba kwa kutumia balbu zilizo na rangi tofauti

Utafutaji unaoanza na "nini"

1. Nini kinachotokea Aleppo?

2. Nini kinachotokea Ethiopia?

3. Nini maana ya 'roho nyekundu'?

4. Ugatuzi ni nini?

5. Candidiasis ni nini?

6. Nausea ni nini?

7. Halitosis ni nini?

8. Pdf ni nini?

9. Mocha ni nini?

10. Detox ni nini?

Maswali ya afya yanayoanza na "jinsi ya"

1. Jinsi ya kupunguza unene

2. Jinsi ya kupata tumbo bapa

3. Jinsi ya kuhesabu siku za ujauzito

4. Jinsi ya kuzuia uvundo kwenye miguu

5. Jinsi ya kupunguza shinikizo la damu

6. Jjinsi ya kutibu mwasho kwenye macho

7. Jinsi ya kuhesabu siku za kushiriki ngono bila kupata mimba

8. Jinsi ya kutibu findo/tonsils

9. Jinsi ya kuongeza unene kwa siku moja

10. Jinsi ya kutibu vidonda vya tumbo