Mbona wanamuziki wamempuuza Trump?

Rais Mteule wa Marekani Haki miliki ya picha AP
Image caption Donald Trump

Ripoti zimeibuka kwamba Rais mteule wa Marekani Donald Trump amekosa wanamuziki nyota ambao watatumbuiza sherehe yake ya kuapishwa hapo mwakani.

Wakati Rais anayeondoka Barack Obama alipokuwa anatawazwa wanamuziki nyota Aretha Franklin na Beyonce waliwatumbuiza maelfu ya watu waliohudhuria kutawazwa kwake.Wakati wa Urais wake, Obama amewaalika kwenye ikulu wanamziki mashuhuri kama vile Rihanna, James Taylor, na Kendrick Lamar.

Inaonekana Rais mpya hana bahati ya kukumbatiwa na wanamziki.

Kamati maalum inayotayarisha kuapishwa kwake imekuwa na wakati mgumu kuwatafuta wanamziki nyota ambao wataimba wakati wa sherehe hiyo ya Januari 20 mwaka ujao.

Baadhi ya duru zimesema wamekuwa wakiwasiliana na mameneja na maajenti wa wanamuziki bila mafanikio yeyote.

Mwamziki John Legend ambaye amealikwa kwenye dhifa kadhaa wakati wa utawala wa Rais Obama amesema hajashangaa kutokana na hali ya sasa.

''Wasanii wote wanachukia dharau, sisi hutaka kuwa na maoni huru'', amesema Legend.

Ameongeza kusema, ''Tukimuona mtu anawagawanya raia na kuchochea chuki na dharau, sidhanii anaweza kuwavutia wasanii maana hawataki kuhusishwa na mtu kama huyu''.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption John Legend amesema wanamziki hawatakubali mwaliko

Kwenye tamasha la tuzo ya BBC ya wananziki {BBC Music Awards} mwanamuziki Zara Larsson alisema, ''Binafsi siwezi kushiriki tamasha la Trump, wanamziki wengi wanamuunga mkono Hillary Clinton, sioni wakibadilisha nia, hilo haliwezekani''.

Licha ya kuwa na wakati mgumu kuwatafuta wanamziki, hata hivyo kamati ya kupanga kuapishwa kwa Rais mteule ilitangaza mafanikio makubwa wezi wa Novemba pale waliposema kumpata mwanamziki Elton John ambae atatumbuiza wakati wa karamu ya jioni.

Hata hivyo siku chache baadaye, Sir Elton John aliandika taarifa za kukanusha hilo na kusema hakukua na ukweli wowote na hawezi kushiriki.

Msanii Kanye West amenukuliwa akisema anamuunga mkono Donald Trump na kwamba japo hakupiga kura, iwapo angefika kituo cha kura angempigia Trump.

Pia mwanamziki huyo amekutana na Rais Mteule hapo Desemba 13.

Wawili hao hawakusema chochote kwa waandishi wa habari ila tu kwamba walikutana kujadili kuhusu maisha, na kwamba walikuwa marafiki.

Wanamziki ambao wametajwa kushiriki shere hiyo ni wale wasio na umaarufu kama Kid Rock, Achy Breaky na Billy Ray Cyrus.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ted Nugent, Kid Rock na Billy Ray Cyrus wanamziki wanaomuunga mkono Donald Trump

Duru zaidi zinasema kamati ya Trump kwa sasa imeanza kuwasihi wanamziki Bruno Mars na Justin Timberlake. Hali imekua mbaya kiasi cha kamati hiyo kukiuka kanuni zilizowekwa na kuwaahidi wasanii kwamba watalipwa ada ya kushiriki.

Duru zinasema kamati hiyo iko tayari kulipa bila kujali gharama. Hata hivyo mwenyekiti wa kamati hiyo Boris Epshteyn amekanusha hilo.

Amesema,''Hizo taarifa siyo kweli, nani huyo amesema kwamba wanakamati wanajihusisha na vitendo kinyume na kanuni?''

Hata hivyo, wengi wanahoji, nani atakubali mwaliko huo hata kama atapokea malipo? ''Sidhani mimi nitachukua pesa kushiriki sherehe hiyo'' Amesema mwanamziki wa Marekani Adam Lambert, ambae ni mtetezi wa haki za wapenzi wa jinsia moja. Lakini mwannamuziki mwenzake Rick Astley ambaye alivuma miaka ya 80 amesema,'' Aaah inategemea unalipwa pesa ngapi''.

Mishipi ya dhahabu

Hata hivyo yeye haungi mkono utawala wa Rais Trump. Ameongeza,''Dunia nzima imeshuhudia kivumbi cha kisiasa na kutishika, sidhani kuna msanii anayetaka kwenda kusherekea na Trump akiapishwa''.

Inaonekana wazi kwamba tasnia ya muziki haivutiwi na Rais mteule.

Mwanamuziki Matt Healy alialikwa kuimba wakati wa kutawazwa kwa Rais wa Marekani mwaka wa 1975.

Hata hivyo aliweka sharti moja, kwanza wamlipe kabla ya kushiriki. Alipoulizwa angetoza nini akasema, ''Nataka mishipi ya dhahabu kwenye viti vya ndege yangu binafsi na dola milioni moja!''.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii