Syria:Maelfu ya watu wapelekwa sehemu salama Aleppo

Maisha mapya baada ya vita
Image caption Maisha mapya baada ya vita

Watu takriban elfu tatu wakiwemo mamia ya watoto wameanza kuokolewa kutoka maeneo yaliyokuwa yanashikiliwa na waasi huko Aleppo.

Kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema watoa misaada kwa sasa wanachukua mamia ya watu kutoka maeneo mbalimbali na kuwapeleka sehemu salama zaidi.

Mlolongo wa magari ya wagonjwa na magari ya abiria yamekuwa yakifanya kazi kubwa kusaidia kuwasogeza watu hao katika sehemu zinazoshikiliwa na serikali.

Image caption Takriban watu 50,000 wanasemekana bado wanaishi Mashariki mwa Aleppo

Maafisa wanasema uokoaji huo unatarajiwa kuchukua siku kadhaa.