Sahihi ya Donald Trump inafichua nini?

Donald Trump and Kanye West Haki miliki ya picha Getty Images

Donald Trump alimweleza Kanye West kuwa "rafiki mkuu" kwenye jalada la nakala ya jarida la Time aliyompa.

Mtaalamu wa miandiko ya watu Elaine Quigley anasema mwandiko wa Donald Trump alipokutana na Kanye West unaonyesha hakubadilisha hisia zake walipokutana.

Anasema uhusiano wao si wa karibu sana kama alivyosema Bw Trump.

Donald Trump alimpa Kanye nakala ya jarida ambapo alitangazwa kuwa mtu mashuhuri zaidi wa mwaka 2016.

Ameandika kwa herufi kubwa na sahihi yake haionekani vyema, inaoenakana kama mchoro.

Haki miliki ya picha KANYE WEST/TWITTER
Image caption Jalada la jarida la Time ambalo Trump aliandika saini yake

Bi Quigley anasema sahihi hiyo inaonyesha mtu ambaye ni "mkali" na inaonesha kwamba Bw trump yuko tayari kwa "mapambano hali ikibidi".

Elaine, ambaye ni mwenyekiti wa taasisi ya wataalamu wa miandiko ya Uingereza, ameambia BBC kwamba kinachojitokeza kwenye mwandiko wa Bw Trump ni picha inaoambia mtu "tahadhari, ninaweza kukuuma ukivuka mpaka."

"Uhusiano wake na Kanye West walipokutana unaonekana kuwa sawa na wakati anapokutana na watu wengine wote na kusalimiana nao. Huwa halegezi msimamo wake au kujitosa ndani sana ya uhusiano na watu wengine ila kwa familia yake."

Elaine anasema kuna mengi pia ya kufahamu kuhusu ujumbe aliomwandikia Kanye.

"Kuna ishara kwamba si mtu wa kufikiria sana, lakini yuko tayari kubadilika na mandhari na majira mambo yanavyobadilika," anasema Elaine.

"Hilo humfaa sana, kwani kutokana na wadhifa wake na cheo chake anahitajika kuchukua hatua kila wakati, ili kuendelea kudhibiti hali."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Donald Trump na Kanye West walikumbatiana wakiagana baada ya mkutano

Elaine anasema mwandiko wa Trump kwenye ujumbe wake kwa Kanye unalingana na tabia yake awali na unafichua jinsi anavyotaka kutazamwa na watu wengine.

"Mistari inayolala kidogo kwenye mwandiko wake ni ishara ya mtu aliye tayari kuchukua hatua, na anataka kuonekana kama mtu aliye tayari na anayeweza kutumia vyema fursa zinapotokea," anasema.

"BwTrump anaonekana kutumia kalamu yenye mwandiko pana, ambao unaonyesha anavyokumbatia maisha na watu wengine.

"Anaweza kuwa rafiki mkuu kwa wale walio karibu naye, lakini pia anaweza kushambulia kwa ukali akihisi kwamba anatishiwa."

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii