Marekani yaapa kuichukulia hatua Urusi

Obama akutana na Putin mjini New York Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Obama akutana na Putin mjini New York

Rais wa Marekania Barack Obama ameapa kuchukua hatua dhidi ya Urusi kwa madai kuwa ilihusika na kushwawishi uchaguzi wa urais nchini Marekani

"Tunahitaji kuchukua hatua na tutafanya hivyo," aliiambia radio ya moja ya Marekani.

Urusi inalaumiwa na Marekani kwa kudukua parua pepe ya chama cha Democratic na za msaidizi wa Hillary Clinton, madaia ambayo Urusi inayakanusha vikali.

Naye rais mteule Donald Trumo ametaja madai hayo kuwa yasiyo ya ukweli na yaliyochochewa kwa misingi ya kisiasa.

Mashirika ya ujasusi ya nasema kuwa yana ushahidi wa kutosha kuwa wadukuzi wa Urusi walio na uhusiano na serikali waliendesha udukuzi huo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption John Podesta, ambaye liongzoa kampeni ya Clinton, email zake zilidukuliwa na kuchapishwa na mtandao wa Wikileaks

Siku ya Alhamisi msemaji wa Ikulu ya White House alisema kuwa Rais Vladimir Putin alihusika na udukuzi huo.

Saa chache baadaye rais Obama alisema, "nafikiri hakuna shaka kuwa wakati serikali yoyote ya kigeni inajaribu kuvuruga uchaguzi wetu, tunahitaji kuchukua hatua na tutafanya hivyo."

"Bwana Putin anafahamu hisia zangu kuhusu hili, kwa sababu nimezungumza naye moja kwa moja."

Haijulikani ni hatua gani Marekani inanuia kuchukua, huku Obama akitarajiwa kuondoka ofisini tarehe 20 mwezi Januari mwakani.

Bwana Trump amewalaumu wanademocrats na kuhusisha Urusi ili kuficha aibu ya kushindwa kwenye uchaguzi.

Trump alikuwa ameonyesha kumpenda Putin na uteuzi wa waziri wake wa mashauri ya nchi za kigeni, mafanyabiashara tajiri Rex Tillerson mabaye amefanya kazi kwa karibu na raia huyo wa Urusi, umezua wasi wasi.