YouTube yafunga akaunti ya televisheni ya Korea Kaskazini

Mwezi Januari mtandao huo ulikuwa ukitangaza habari za majario ya mabomu ya nuklia. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mwezi Januari mtandao huo ulikuwa ukitangaza habari za majario ya mabomu ya nuklia.

Mtandao wa video wa YouTube umefunga akaunti ya mtandoa huo inayotumiwa na shirika la habari la Televisheni la Korea Kaskazini.

Ujumbe unaoonekana kwenye akaunti hiyo unasema kuwa umefungwa kwa kukiuka kanuni za YouTube.

Akaunti hiyo hutumiwa kutangaza matukio ya kila siku.

Ripoti zinasema kuwa sababu kuu ya kufungwa akaunti hiyo ni kuwa Korea Kaskazini ilikuw ikipata malipo ya biashara kupitia akaunti hiyo ambayo inaweza kukiuka vikwazo vya Marekani.

Kwa mujibu wa gazeti la Washington Post, akaunti hiyo ilifungwa mwezi uliopita na mtandoa wa Google ili kuzuia kukiuka vikwazo.

Google haitamki lolote kuhusu hatua hiyo lakini hata hivuo imesema kuwa hufunga mitandao ambayo hukiuka kanuni za mtandao wa YouTube wakati inahitajika kufanya hivyo kisheria.

Mwezi Januari mtandao huo ulikuwa ukitangaza habari za majario ya mabomu ya nuklia.

Haki miliki ya picha YouTube/Korean Central Television
Image caption Akaunti ya televisheni ya Korean Kaskazini iliyofungwa