Bolasie kufanyiwa upasuaji wa pili

Yannick Bolasie Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Yannick Bolasie

Wing'a wa klabu ya Everton Yannick Bolasie anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa goti mwaka ujao.

Bolasei mwenye umri wa miaka 27 alijeruhiwa wakati wa mechi kati ya Everton na Manchester United tarehe 4 mwezi huu.

Meneja wa Everton Rodald Koemen anasema kwa mchezaji huyo kutoka DR Congo alifanyiwa upasuaji wa kano za goti siku ya Alhamis

kwa sasa anahitaji muda wa hadi majuma 10 ili kuweza kufanyiwa upasuaji wa pili.

Koeman anasema kuwa Bolasie ambaye alijunga Everton kutoka Crystal Palace mwezi Agosti atakaa benchi kwa muda mrefu na hatachezaakatika mechi ya kwanza ya kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika nchini Gabon mwezi ujao.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Yannick Bolasie alipata jeraha akimkabili Antony ,Martial wa Man U

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii

Kuhusu BBC

Mitandao inayohusiana

BBC haina haihusiki vyovyote na taarifa za mitandao ya kujitegemea