Duterte aitaka Marekani iondoe wanajeshi Ufilipino

Duterte ataka Marekani iwaondoe wanajeshi wake Ufilipino Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Duterte ataka Marekani iwaondoe wanajeshi wake Ufilipino

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameiambia Marekani ijiandae kuondoa wanajeshi wake nchini Ufilipino.

Bwana Duterte amesema huenda akafanyia marekebisho muafaka wa kijeshi uliyofikiwa kati ya mataifa hayo,ambayo inawaruhusu maelfu ya wanajeshi wa Marekani kuwa nchini humo kisheria.

Rais huyo hata hivyo ,amesema uhusianao kati ya mataifa hayo mawili huenda ukaimarika chini ya utawala wa Donald Trump.

Habari zaidi zinasema matamshi Duterte huenda yamechangiwa na uamuzi wa Marekani kusitisha msaada wake kwa Ufilipino kufuatia sera yake ya kuwapiga risasi na kuwaua wahalifu wa ulanguzi wa dawa za kulevya.