Clinton alipata kura nyingi kuliko za Obama

Clinton alipata kura nyingi zaidi kuliko mgombea yeyote mzungu nchini Marekani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Clinton alipata kura nyingi zaidi kuliko mgombea yeyote mzungu nchini Marekani

Baada ya kura zote kuweka pamoja imebainika kuwa Bi Hillary Clinton, ambaye alishindwa na Donald Trump alikuwa amepata kura nyingi zaidi kuliko Barack Obama wakati wa ushindi wake wa mwaka 2012 .

Amemshinda Trump kwa karibu kura milioni 2.8.

Uongozi huo wa Bi Clinton ndio mkubwa zaidi katika ushindi tano kutoka kwa wagombea watano wa urais, ambao walishinda kwa kura nyingi lakini wakashindwa kuwa marais.

Kando na ushindi wa Obama wa mwaka 2008, Bi Clinton amepata kura nyingi kuliko rais yeyote katika historia ya Marekani

Marekani imeshuhudia kuongezeka kwa idadi ya watu katika karne iliyopita, ambayo huenda ikawa sababu Bi Clinton alipata kura nyingi zaidi kuliko wagombea wa awali.

Mwaka huu Marekani ilikuwa na wapiga kura waliosajiliwa milioni 200 kwa mara ya kwanza katika historia.

Mara ya mwisho mgombea alishindwa kwa kura nyindi lakini akakosa kuibuka mshindi wa urais ni mwaka 2000 wakati Rais Bush alishindwa na Al Gore kwa kura 500,000 lakini akanafikiwa kuingia ikulu.

Tofauti ya kura za Clinton milioni 2.5 hata hivyo ni ya chini ikilinganishwa na kura milioni 3 za George W Bush dhidi ya John Kerry mwaka 2004.

Uchaguzi wa mwaka 2004 ulikuwa na wapiga kura wengi zaidi kuliko wa mwaka 2016 kwa asilimia 1.7.

Ikiwa uchaguzi wa mwaka 2016 ungekuwa na asilimia sawa hiyo basi watu milioni 2 zaidi wangepiga kura.