Trump aitaka China kuhifadhi manuwari ya Marekani

Rais mteule wa Marekani Donald Trump
Image caption Rais mteule wa Marekani Donald Trump

Rais mteule wa Marekani Donald Trump ,amesema kuwa Marekani inafaa kuiomba China kuiweka manuwari ya Marekani iliopatikana katika bahari ya kusini mwa taifa hilo.

Awali Trump alikuwa ameishutumu Beijing kwa kuiba manuwari hiyo katika maji ya kimataifa.

China iliichukua manuwari hiyo katika pwani ya Ufilipino wakati meli za wanamaji wa Marekani zilipojaribu kuichukua, hatua ilioikasirisha Marekani.

China imesema kuwa itaikabidhi Marekani, lakini matamshi ya Trump huenda yakatatiza mpango huo.

China yakamata chombo cha Marekani baharini

Marekani yatuliza China juu ya Taiwan

Hii ni mara ya tatu katika wiki kadhaa kwa yeye kukosana na China.

Wakati huohuo Trump amekamilisha ziara yake ya wiki tatu ya kusherehekea ushindi , katika mji ulioshuhudia mkutano mkubwa zaidi wakati wa kampeni zake.

Image caption Manuwari ya Marekani iliopataikana kusini mwa bahari ya China

Alipowasili katika mji wa Mobile, Alabama, Trump alikaribishwa na kundi la wanawake waliovalia mavazi ya kitamaduni yanayovaliwa na jamii za kusini mwa Marekani.

Katika uwanja uliojaa pomoni, Trump aliahidi kwamba atatimiza ahadi yake ya kujenga ukuta kwenye mpaka wa Mexico na Marekani.

Trump ataapishwa tarehe 20 mwezi Januari.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii