Uchaguzi: Usalama waimarishwa Ivory Coast

Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rais Allasane Ouattara wa Ivory Coast

Maafisa wa usalama wapatao 30,000 wamesambazwa kote nchini Ivory Coast kabla ya kuanza kwa uchaguzi wa ubunge hii leo, hata baada ya kipindi cha amani cha kampeni.

Rais Alassane Ouattara amewaomba raia wa taifa hilo kuunga mkono chama chake, the Rally of Republicans.

Upinzani ulisusia Uchaguzi wa ubunge miaka 5 iliyopita, kufuatia machafuko ya kisiasa yaliyodumu miezi kadhaa, na kupelekea vifo vya watu 3000.