Mpiganaji wa IS awaua wanajeshi 48 Yemen

Eneo la tukio la shambulio ambapo wanajeshi 40 waliuawa nchini Yemen Haki miliki ya picha AFP
Image caption Eneo la tukio la shambulio ambapo wanajeshi 40 waliuawa nchini Yemen

Mshambuliaji wa kujitolea kufa katika mji wa bandarini Aden amewauwa wanajeshi 48 na kuwajeruhi wengine wengi.

Ripoti zinasema kwamba wanajeshi hao walikuwa wamepanga foleni kupokea mishahara yao karibu na kambi ya wanajeshi, wakati mshambuliaji huyo alipojilipua.

Wiki iliyopita, wapiganaji wa Islamic state waliwaua wanajeshi 50 mjini Aden, ambao wako chini ya udhibiti wa serikali inayotambuliwa kimataifa ya Yemen.

Islamic State limekiri kutekeleza shambulio hilo ambalo linasema limewaua ''waasi'' 70.

Shambulio hilo linajiri wiki moja baada ya shambulio jingine kama hilo kuwaua wanajeshi 48 katika kambi hiyo