Waasi wachoma mabasi ya uokoaji watu Syria

Mabasi ya kuwaokoa watu yamechomwa na waasi nchini Syria Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mabasi ya kuwaokoa watu yamechomwa na waasi nchini Syria

Mabasi kadhaa yaliokuwa yakielekea kuwaokoa wagonjwa na watu waliojeruhiwa katika kijiji kinachomilikiwa na serikali katika mkoa wa Idlib nchini Syria yamechomwa na waasi.

Msafara huo ulikuwa ukielekea Foah na Kefraya maeneo yaliozungukwa na waasi.

Vikosi vinavyounga mkono serikali vinataka watu kuruhusiwa kuondoka katika kijiji cha Shia ili uokozi wa watu waliopo Allepo uanze.

Maelfu ya watu wanatarajia kuondoka .

Mpango wa awali wa kuwaondosha watu mashariki mwa Aleppo ulifeli siku ya Ijumaa, ukiwaacha raia wakiwa wamekwama katika vituo tofauti bila chakula na makao.