Uchaguzi Ivory Coast: Upigaji kura wachelewa

Uchaguzi nchini Ivory Coast waanza kuchelewa
Image caption Uchaguzi nchini Ivory Coast waanza kuchelewa

Upigaji kura umechelewa kuanza katika maeneo kadhaa ya Ivory Coast, katika uchaguzi wa wabunge, kwa sababu za usafiri.

Raia zaidi ya milioni 6 wataamua iwapo watampa kura nyingi rais Alassane Ouattara na serikali ya mseto, kama alivowaomba.

Tofauti na uchaguzi wa miaka mitano iliyopita, karibu upinzani wote unashiriki katika uchaguzi huu, pamoja na tawi moja la chama cha rais wa zamani, Laurent Gbagbo.

Laurent Gbagbo, anafanyiwa kesi na mahakama ya Kimataifa, ICC, kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.