Wekundu wa Msimbazi waongoza ligi

Simba Haki miliki ya picha Google
Image caption Wachezaji wa kikosi cha timu ya Simba

Ligi kuu ya Tanzania bara mzunguko wa pili imeendelea tena kwa michezo minne kuchezwa katika viwanja vinne tofauti.

Wekundu wa Msimbazi Simba walipata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Ndanda fc.

Kwa ushindi huo Simba wamerejea kileleni mwa ligi wakiwa na alama 38 huku watani wao wa jadi Yanga wakiwa katika nafasi ya pili kwa alama 36.

Katika michezo mingine Mbao Fc walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Stand United.

Wanalambalamba Azam watoshana nguvu na African kwa sare ya bila kufungana huku Tanzania Prison wakiwatambia Majimaji kwa kuwachapa bao 1-0.