Man City yaichapa Arsenal 2-1

Arsenal Haki miliki ya picha PA
Image caption Beki wa Arsenal Hector Bellerin akikabilina na winga wa Manchester City Raheem Sterling

Matajiri wa jiji la Manchester, Man City wakicheza katika dimba lao Etihad wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Arsenal.

Arsenal ndio walianza kupata goli katika dakika ya 5 ya mchezo kupita kwa Theo Walcott.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wachezaji wa Arsenal wakishanglia goli la Theo Walcott

Man City walisawazisha goli hilo katika pindi cha pili dakika ya 47 bao likiwekwa kambani na Leroy Sane.

Bao la ushindi la vijana wa Pep Guardiola lifungwa na winga Raheem Sterling katika dakika ya 71 ya mchezo.

Hiki ni kipigo cha pili mfululizo kwa Arsenal baada ya katikati ya wiki kupigwa 2-1 na Everton

Katika michezo mingine Tottenham iliichapa Burnley 2-1 na Southampton walipata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Bournemouth.

Jumatatu Usiku kutapigwa dabi ya Merseyside. Ambapo Everton wataalika Liverpool katika dimba la Goodison Park