Timu za vijana za Tanzania zapewa majina

Haki miliki ya picha Google
Image caption Kikosi cha timu ya vijana ya Tanzania

Timu za taifa za Tanzania za umri chini ya miaka 23 kwa wanaume na wanawake ambazo hazikuwa na majina sasa zinaitwa Kilimanjaro Warriors (wanaume) wakati wanawake ni Kilimanjaro Starlets.

Uteuzi wa majina hayo umefanywa na Kamati ya utendaji ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF.

Timu hizo ambazo ni maalumu kwa ajili ya michuano ya Olimpiki zitaanza maandalizi yake Januari mwakani.

wachezaji watakaounda timu hizo zinazojiandaa kwa ajili ya michuano ya Olimpiki itakayofanyika Japan, mwaka 2020 watatoka katika timu za sasa za wachezaji wenye umri chini ya miaka 20.

Mechi za mchujo kwa ajili ya michuano