Ndege ya Urusi yaanguka Siberia

Ramani ya Urusi

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema ndege aina ya IL-18 imeanduka eneo la Yakutia, Siberia ikiwa na watu 39.

Maafisa wa wizara hiyo wamesema watu 16 wamejeruhiwa vibaya, na kukanusha taarifa za awali kwamba watu 27 walikuwa wamefariki.

Ndege hiyo ilikuwa na abiria 32 na wahudumu saba ilipoanguka karibu na Tiksi katika wilaya ya Bulun, mashariki mwa Urusi.

Eneo hilo linadaiwa kuwa na hali mbaya ya hewa ajali hiyo ilipotokea.

Ndege hiyo ilikuwa kwenye safari ya kawaida kutoka Kansk ilipoanguka kilomita 30 kabla ya kufika Tiksi saa 19:45 GMT Jumapili.

Ndege hiyo ilivunjika vipande vitatu.

Taarifa zinadokeza huenda ilijaribu kutua kwa dharura.

Helikopta aina ya Mi-8 zimetumwa eneo la ajali.

Pamoja na watu 16 waliojeruhiwa vibaya, watu wengine saba wamehitaji matibabu hospitalini.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii